Kwa sasa bongo ukizungumzia watayarishaji wa muziki wa kizazi kipya
wanaofanya vizuri huwezi kuacha kumzungumzia Messen kutoka D Fatality
Music,ambaye anafanya kazi zake hapo,Kipindi cha nyuma Messen alikuwa
anafanyia kazi zake sebuleni kwao, ambapo alikuwa anapata shida wakati
akiwa anataka hasa kuingiza vocal, hapo ni lazima madirisha yafungwe na
kila mtu akae kimya.
Lakini siku kadri zilivyozidi kwenda na kazi zinafanyika za maana kwa
mujibu wa Messen ikabidi afanye mpango wa kutengeneza ofisi yake kwao
hapo hapo, ambapo hadi sasa ameshagharamikia takribani milioni 30 katika
ujenzi na vifaa vya studio lakini bado haijakamilika kama anavyotaka
iwe.
没有评论:
发表评论