2014年8月11日星期一

TUPO KWENYE MAREKEBISHO MADOGOMADOGO SAMAHANI KWA USUMBUFU WOWOTE UTAKAOJITOKEZA

BY  UONGOZI.

2014年6月16日星期一

RAPPER MKALI WA KIKE EVE AOLEWA.

Rapper wa kike Eve hatimaye amefunga ndoa na mpenzi wake aitwae Maxmillion Cooper, June, 13 huko Ibiza, Hispania.

Hii ni ndoa ya kwanza kwa rapper huyo mwenye umri wa miaka 35 lakini mumewe ana watoto wanne ambao alizaa na mkewe wa zamani.

Eve na Cooper walikuwa kwenye uhusiano kwa kipindi cha miaka 4 na walichumbiana rasmi mwaka jana, katika sikukuu ya Christmas.

Cooper ambaye ni raia wa Uingereza mwenye umri wa miaka 41, ni mfanyabiashara na dereva wa mbio za magari mwenye utajiri wenye thamani ya dola za kimarekani milioni 50.  

Wanandoa hao walitoa tamko la pamoja kuwashukuru wageni waalikwa:
“Tunafuraha iliyopitiliza kusherehekea ndoa na marafiki zetu wote na familia na kuanza safari yetu katika maisha mapya pamoja. Imekuwa experience nzuri sana na tunafuraha hata zaidi ya tulivyofikiria ingekuwa. Asanteni kwa kututakia maisha mema.”

D'BANJ AKANA KUWA NA MAHUSIANO NA MREMBO GENEVIEVE.

Wengi wanaamini kuwa DBanj aliwahi kukiri kwenye nyimbo zake kuwa anampenda muigizaji wa Nollywood Genevieve Nnaji na hata watu wa karibu wa Geneveive walikaririwa hivi karibuni wakisema kuwa wawili hao ni wapenzi.

DBanj amekana wazi kuwa na uhusiano na muigizaji huyo katika mahojiano aliyofanya na Vanguard.

“Kumekuwa na tetesi nyingi sana kuhusu mambo mengi. Sipendi kabisa kuzungumzia uhusiano wangu binafsi kwa sababu siku zote watu wananielewa tofauti. Lakini daima tetesi zitabaki kuwa tetesi.”

“Kwa kweli sina uhusiano wa mapenzi na Geneveive. Ngoja niweke mambo sawa.” Amesema DBanj.

Alipoulizwa kama waliwahi kuwa na ukaribu na kutaka kuwa wapenzi alidai yeye binafsi hajawahi kufikia huko.

DBanj ambaye hivi sasa amefikisha umri wa miaka 34 aliulizwa kuhusu mpango wa kuoa na kutulia na familia na hapo majibu yake yalikuwa tata.

“Ofcourse, ninawaza kuhusu kutulia. Nani kasema sijafunga ndoa? Maisha yangu binafsi lazima yabaki kuwa faragha, hususani kwa vyombo vya habari.”
Ndipo muuliza maswali alipouliaz, “Inamaana kuwa DBanj alifunga ndoa kwa siri?”

Dbanj akajibu, “Inaweza kuwa hivyo.”

RIHANNA ANATAMANI SANA KUWA NA MTOTO KWA SASA.

Rihanna hivi sasa ameonesha upande wa pili wa maisha yake kama mwanamke wa kawaida anaetamani kuwa mama wa mtoto tofauti na maisha ya ustaa na kula bata.

Mwimbaji huyo hivi sasa ameonekana kutumia muda wake mwingi kukaa na kichanga wa mdogo wake huku akimuonesha malezi yote kama mama yake mzazi kasoro kumnyonyesha.

Mdogo wake ameamua kuwapa jina la utani Rihanna na mwanae ‘Pinky and the bail’ na anasema sababu kubwa ya kuwapa jina hilo ni kuwa wao hupenda kuangalia cartoon badala ya kombe la dunia na wanalala pamoja.

Huenda Rihanna akayazoea maisha ya mama na kuamua kuwa kama Ciara, Lil Kim na Beyonce ambao wao tayari ni akimama.

2014年6月10日星期二

UNAJUA ILIKUWAJE DIAMOND ALIVYOINGIA STUDIO NA MAFIKIZOLO SOMA HAPA...

diamond mafikizolo
Diamond Platinumz ana kila sababu ya kuikumbuka na kujivunia kupendekezwa kuwania tuzo za MTV MAMA 2014 ingawa hakushinda tuzo yoyote.

Tuzo hizo zimemkutanisha na kundi la Mafikizolo linalofanya vizuri Afrika na kufanya mazungumzo kuhusu kufanya kazi pamoja. Mazungumzo hayo yalifanikiwa na wakaamua kupiga kazi.

Mafikizolo waliambatana na Diamond na meneja wake (Babu Tale) hadi jikoni wanakopikia hits zao zote na wakamkutanisha na mpishi wa hits hizo, producer Oskido. Kazi ilifanyika kuanzia idea, mdundo, melodies hadi kukamilisha session. 

 Bila shaka hapo aliongeza maarifa zaidi  kuhusu ufanyaji wake wa kazi, lakini pia kundi hilo lilimtia moyo zaidi baada ya kumpigia makofi wakati anafanya vocals.

Wimbo ulikamilika na kila mmoja akajiridhishs kuwa ni the next hit ya Afrika ingawa hawakuipa jina.


2014年6月5日星期四

JUSTIN BIEBER AONEKANA TENA AKITUMIA MANENO YA UBAGUZI.

Wiki hii haijamuendea vizuri mwimbaji wa Canada, Justin Bieber ambaye ameripotiwa kuonekana kwenye video nyingine akitumia maneno yenye ubaguzi wa rangi ikiwa ni siku moja baada ya kuomba radhi kwa video ya aina hiyo iliyotolewa na TMZ.

Katika video hiyo yenye dakika 45 iliyotolewa na The Sun ambayo pia ilichukuliwa wakati akiwa na umri mdogo, Bieber anasemekana kuwa alibadili mashairi ya wimbo wake wa ‘One Less Lonely Girl’ na kuuita ‘One Less Lonely Nig**’.

Chanzo kimeiambia NY Dailye News kuwa Bieber alifanya utani kuhusu kutaka kujiunga na kundi la kibaguzi lilikuwa likiwapiga vita watu weusi la Ku Klux Klan.

“Inabidi watu walilione hili. Watoto wa kawaida katika jamii hawafanyi utani wa aina hii. Analindwa na watu wa mitandao lakini kamera hazidanganyi. Huyu ni Justin halisi.”