Rihanna hivi sasa ameonesha upande
wa pili wa maisha yake kama mwanamke wa kawaida anaetamani kuwa mama wa mtoto
tofauti na maisha ya ustaa na kula bata.
Mwimbaji huyo hivi sasa ameonekana
kutumia muda wake mwingi kukaa na kichanga wa mdogo wake huku akimuonesha
malezi yote kama mama yake mzazi kasoro kumnyonyesha.
Mdogo wake ameamua kuwapa jina la
utani Rihanna na mwanae ‘Pinky and the bail’ na anasema sababu kubwa ya kuwapa
jina hilo ni kuwa wao hupenda kuangalia cartoon badala ya kombe la dunia na
wanalala pamoja.
Huenda Rihanna akayazoea maisha ya
mama na kuamua kuwa kama Ciara, Lil Kim na Beyonce ambao wao tayari ni akimama.
没有评论:
发表评论