2014年6月10日星期二

UNAJUA ILIKUWAJE DIAMOND ALIVYOINGIA STUDIO NA MAFIKIZOLO SOMA HAPA...

diamond mafikizolo
Diamond Platinumz ana kila sababu ya kuikumbuka na kujivunia kupendekezwa kuwania tuzo za MTV MAMA 2014 ingawa hakushinda tuzo yoyote.

Tuzo hizo zimemkutanisha na kundi la Mafikizolo linalofanya vizuri Afrika na kufanya mazungumzo kuhusu kufanya kazi pamoja. Mazungumzo hayo yalifanikiwa na wakaamua kupiga kazi.

Mafikizolo waliambatana na Diamond na meneja wake (Babu Tale) hadi jikoni wanakopikia hits zao zote na wakamkutanisha na mpishi wa hits hizo, producer Oskido. Kazi ilifanyika kuanzia idea, mdundo, melodies hadi kukamilisha session. 

 Bila shaka hapo aliongeza maarifa zaidi  kuhusu ufanyaji wake wa kazi, lakini pia kundi hilo lilimtia moyo zaidi baada ya kumpigia makofi wakati anafanya vocals.

Wimbo ulikamilika na kila mmoja akajiridhishs kuwa ni the next hit ya Afrika ingawa hawakuipa jina.


没有评论:

发表评论