Wiki hii haijamuendea vizuri
mwimbaji wa Canada, Justin Bieber ambaye ameripotiwa kuonekana kwenye video
nyingine akitumia maneno yenye ubaguzi wa rangi ikiwa ni siku moja baada ya
kuomba radhi kwa video ya aina hiyo iliyotolewa na TMZ.
Katika video hiyo yenye dakika 45
iliyotolewa na The Sun ambayo pia ilichukuliwa wakati akiwa na umri mdogo,
Bieber anasemekana kuwa alibadili mashairi ya wimbo wake wa ‘One Less Lonely
Girl’ na kuuita ‘One Less Lonely Nig**’.
Chanzo kimeiambia NY Dailye News
kuwa Bieber alifanya utani kuhusu kutaka kujiunga na kundi la kibaguzi lilikuwa
likiwapiga vita watu weusi la Ku Klux Klan.
“Inabidi watu walilione hili. Watoto
wa kawaida katika jamii hawafanyi utani wa aina hii. Analindwa na watu wa
mitandao lakini kamera hazidanganyi. Huyu ni Justin halisi.”
没有评论:
发表评论