Wengi wanaamini kuwa DBanj aliwahi
kukiri kwenye nyimbo zake kuwa anampenda muigizaji wa Nollywood Genevieve Nnaji
na hata watu wa karibu wa Geneveive walikaririwa hivi karibuni wakisema kuwa
wawili hao ni wapenzi.
DBanj amekana wazi kuwa na uhusiano
na muigizaji huyo katika mahojiano aliyofanya na Vanguard.
“Kumekuwa na tetesi nyingi sana
kuhusu mambo mengi. Sipendi kabisa kuzungumzia uhusiano wangu binafsi kwa
sababu siku zote watu wananielewa tofauti. Lakini daima tetesi zitabaki kuwa
tetesi.”
“Kwa kweli sina uhusiano wa mapenzi
na Geneveive. Ngoja niweke mambo sawa.” Amesema DBanj.
Alipoulizwa kama waliwahi kuwa na
ukaribu na kutaka kuwa wapenzi alidai yeye binafsi hajawahi kufikia huko.
DBanj ambaye hivi sasa amefikisha
umri wa miaka 34 aliulizwa kuhusu mpango wa kuoa na kutulia na familia na hapo
majibu yake yalikuwa tata.
“Ofcourse, ninawaza kuhusu kutulia.
Nani kasema sijafunga ndoa? Maisha yangu binafsi lazima yabaki kuwa faragha,
hususani kwa vyombo vya habari.”
Ndipo muuliza maswali alipouliaz,
“Inamaana kuwa DBanj alifunga ndoa kwa siri?”
Dbanj akajibu, “Inaweza kuwa hivyo.”
没有评论:
发表评论