Rapper wa kike Eve hatimaye amefunga
ndoa na mpenzi wake aitwae Maxmillion Cooper, June, 13 huko Ibiza, Hispania.
Hii ni ndoa ya kwanza kwa rapper
huyo mwenye umri wa miaka 35 lakini mumewe ana watoto wanne ambao alizaa na
mkewe wa zamani.
Eve na Cooper walikuwa kwenye
uhusiano kwa kipindi cha miaka 4 na walichumbiana rasmi mwaka jana, katika
sikukuu ya Christmas.
Cooper ambaye ni raia wa Uingereza
mwenye umri wa miaka 41, ni mfanyabiashara na dereva wa mbio za magari mwenye
utajiri wenye thamani ya dola za kimarekani milioni 50.
Wanandoa hao walitoa tamko la pamoja
kuwashukuru wageni waalikwa:
“Tunafuraha iliyopitiliza
kusherehekea ndoa na marafiki zetu wote na familia na kuanza safari yetu katika
maisha mapya pamoja. Imekuwa experience nzuri sana na tunafuraha hata zaidi ya
tulivyofikiria ingekuwa. Asanteni kwa kututakia maisha mema.”
没有评论:
发表评论