2014年5月30日星期五
RIPOTA AMPIGA BRAD PITT USONI SIKU YA UZINDUZI WA FILAMU MPYA YA ANGELINA JOLIE.
Muigizaji Brad Pitt alijikuta katika wakati
mgumu Jumanne iliyopita katika uzinduzi wa filamu mpya ya mchumba wake Angeline
Jolie inayoitwa ‘Maleficent’, baada ya kupigwa usoni na ripota wa TV
ambaye ni raia wa Ukraine.
TAZAMA LULU ALIVYOSAHAU KUFICHA CHAKULA YA MTOTO ALAFU ANATEMBEA BARABARANI .
Tukio hilo
lilitokea hivi karibuni katika kiwanja kimoja kichopo mjini Arusha ambapo mmoja
wa watu aliyemtia machoni Lulu aliyeomba hifadhi ya jina lake alisema:
“Yaani
nilimuona Arusha akiwa amevaa gauni lililoacha wazi matiti yake, kaficha chuchu
tu na inavyoonekana gauni lilimvuka, akaonekana akihangaika kulirudishia bila
mafanikio.”
MUME WA MUIMBAJI MAARUFU WA NYIMBO ZA DINI FLORA MBASHA ATUHUMIWA KUMBAKA SHEMEJI YAKE
Mume wa muimbaji wa injili Flora
Mbasha, Emmanuel Mbasha ambaye pia ni muimbaji anatafutwa na jeshi la polisi
kwa tuhuma za kumbaka shemeji yake mwenye umri wa miaka 17.
Kwa mujibu wa Global Publishershers,
mwanaume huyo anasakwa na jeshi la polisi baada ya shemeji yake kuripoti katika
kituo cha polisi Jumatatu wiki hii majira ya mchana na kufungua mashitaka dhidi
ya mwanaume huyo akidai kuwa alimmbaka kwa nyakati tofauti katika siku mbili
(Ijumaa na Jumapili) ya wiki iliyopita nyumbani kwa Mbasha, Tabata-Kimanga, Dar
es Salaam.
Imeelezwa kuwa mlalamikaji
alifanyiwa kitendo hicho Jumamosi sebuleni kwa Mbasha, na Jumapili ndani ya
gari la mlalamikiwa na kwamba kutokana na maumivu makali aliyosababishiwa
aliamua kuripoti katika kituo cha polisi na kufungua kesi yenye Kumbukumbu Na.
TBT/RB/3191/2014 na ya Jalada la Uchunguzi Na. TBT/IR/1865/2014.
Taarifa hizo zimeeleza kuwa kulikuwa
na ugomvi mkubwa kati ya Flora na mumewe hali iliyomsababiha Flora kuondoka
nyumbani na kuishi hotelini na nafasi hiyo mumewe aliitumia kufanya tukio hilo.
Global Publishers imeeleza kuwa
ilizungumza na mlalamikaji kwa njia ya simu na alithibisha kufanyiwa kitendo
hicho na mume wa Flora na kueleza kuwa tayari wameshatoa taarifa polisi.
Jumapili (May 25) ambayo mlalamikaji
anadai alibakwa ndani ya gari na Emmanuel, Flora Mbasha alipost kwenye ukurasa wake wa Facebook picha mbalimbali za matukio
mbalimbali akiwa na mumewe, huku picha ya mwisho ikimuonesha mume wake huyo
akiwa nje ya hospitali ya kanisa huko Haydom, Mbulu (Haydom Lutheran Hospital)
na kuandika ‘Haydom’.
Hata hivyo, tangu kuwepo na tuhuma
hizo mwimbaji huyo wa kike hajapost chochote kwenye Facebook.
Jeshi la polisi bado halijatoa tamko
rasmi kuhusu tukio hilo.
LADY JAY DEE KUCHEZA NA WATOTO KWENYE TAMASHA LA WATOTO EXTEREME KID'S FESTIVAL MAY 31 NA JUNE 1, KATIKA VIWANJA VYA LEADERS CLUB DAR.
Tamasha kubwa la watoto ‘Extreme
Kids Festival’ litakalofanyika May 31 na June 1 katika viwanja vya Leaders
Club, Dar es Salaam na litapambwa na mwimbaji mkongwe wa kike anaependwa sana,
Lady Jay Dee.
Lady Jay Dee atajumuika na watoto
watakaohudhuria tamasha hilo, atawaongoza kuimba nyimbo mbalimbali ili
kuwahamasisha kuonesha vipaji vyao na atawapa zawadi wale watakaofanya vizuri
zaidi.
“Watoto Mambo vipi, Jay Dee
nawakaribisha watoto wote pamoja na wazazi na walezi. Mje basi katika Extreme
Kids Festival. Ni Jumamosi ya tarehe 31 May, si hapo tu na Jumapili ya
tarehe 1 June. Tunatoa nafasi kwa watoto kuzindua vipaji vyao vya kuimba na
washindi watapata zawadi.” Amesema Lady Jay Dee kwenye maelezo yake.
Katika tamasha hilo, mbali na
michezo/games mbalimbali inayopendwa zaidi na watoto pia kutakuwa na semina
fupi kwa ajili ya wazazi na walezi kwa ajili ya kuboresha malezi ya watoto.
Kutakuwa pia na bidhaa mbalimbali
huduma muhimu bora zaidi kwa ajili ya watoto na wanafamilia zitatolewa kwa siku
hizo mbili.
Waandaaji wa Extreme Kids Festival
wamesisitiza kuwa kutakuwa na usalama wa kutosha kwa ajili ya watoto na wote
watakaohudhuria na kwamba hakutakuwa na pombe .
2014年5月22日星期四
SIFA ZA MWANAMKE ATAKAEOLEWA NA YEYE NI........SOMA HAPA
STAA wa filamu Bongo, Yusuf Mlela ametoa kioja cha aina yake
baada ya kufunguka kuwa akifika hatua ya kuingia kwenye ndoa anataka mwanamke
atakayemzidi umri.
Tofauti na
vijana wengine ambao wanapenda kuoa wake wadogo kwao, Mlela alisema anaamini
mwanamke akimzidi umri ndoa itadumu na maisha yao yatakuwa mazuri kwani atakuwa
tayari ameshakomaa kiakili na atakuwa na uwezo mkubwa wa kuiendesha familia.
“Nahitaji mwanamke anayenizidi umri na sitaki nimzidi mimi naamini huyo tutaelewana na ndoa itadumu, sitaki mwanamke ninayemzidi umri mimi maana itakuwa shida kwani sijapangilia hivyo,” alisema Mlela.
“Nahitaji mwanamke anayenizidi umri na sitaki nimzidi mimi naamini huyo tutaelewana na ndoa itadumu, sitaki mwanamke ninayemzidi umri mimi maana itakuwa shida kwani sijapangilia hivyo,” alisema Mlela.
订阅:
博文 (Atom)