RIPOTA AMPIGA BRAD PITT USONI SIKU YA UZINDUZI WA FILAMU MPYA YA ANGELINA JOLIE.
Muigizaji Brad Pitt alijikuta katika wakati
mgumu Jumanne iliyopita katika uzinduzi wa filamu mpya ya mchumba wake Angeline
Jolie inayoitwa ‘Maleficent’, baada ya kupigwa usoni na ripota wa TV
ambaye ni raia wa Ukraine.
Ripota hiyo kazi yake kubwa katika TV ni
kuwatania kwa vitendo watu maarufu kwa kupanga matukio na kisha kurekodi na
kuonesha jinsi wanavyo-react (Prankster).
Hata hivyo, ripota huyo aliyetajwa kwa jina
la Vitalii Sediuk, hakuonesha nia ya utani wakati wakiwa katika red carpet
baada ya kuupenya umati na kumpiga usoni Brad Pitt na kuvunja miwani yake ya
jua.
Walinzi waliingilia kati na kumdhibiti Sediuk
na kisha kumkamata na kumfikisha kwenye vyombo vya sheria.
Vyombo vya usalama vimetoa amri ya dharura
ili kumlinda Brad Pitt na amri hiyo inamtaka Sediuk kukaa mbali na Brad Pitt,
umbali usiopungua hatua 500 kwa muda wa siku tano zijazo.
Ripota huyo mwenye umri wa miaka 25 amefanya
tukio hilo wakati ambapo bado yuko kwenye kipindi cha matazamia (Probation) kwa
tukio alilolifanya mwaka 2013 kutaka kuingilia hotuba iliyokuwa ikitolewa na
Adele kwenye tuzo za Grammy.
Chanzo kimeiambia TMZ kuwa file la kesi yake
limepele kwa muendesha mashitaka wa Los Angeles na kwamba anaweza kukabiliwa na
kesi ya jinai.
没有评论:
发表评论