MFUNGWA MMOJA AWASHITAKI JAY Z,BEYONCE,KANYE WEST,RIHANNA NA CHRIS BROWN, AMESEMA WAMEMUIBIA NYIMBO 3,000 AKIWA GEREZANI.
Katika hali isiyo ya kawaida, polisi wa
California wamepokea mashitaka toka kwa mfungwa mmoja akiwashitaka wanamuziki
wakubwa wa hip hop, na R&B akiwadai fidia ya $ bilioni 2.
Katika faili la kesi hiyo, mtu huyo
aliyefahamika kwa jina la Richard Dupree amewataja Beyonce, Jay Z, Kanye West,
Rihanna na Chris Brown kuwa walimuibia mashairi ya nyimbo zake 3,000
alizoandika wakati akiwa gerezani.
Kwa mujibu wa huffingtonpost, Dupree
alifungua mashitaka katika mahakama ya wilaya ya mashariki mwa California April
21, na anaamini kuwa Beyonce na Jay Z walifanya kazi na CIA, FBI na vitengo
vingine vya ulinzi wa Marekani kumpeleleza na kuyapata mashairi yake.
Anaamini kuwa Chris Brown, Kanye West na
Rihanna walihusika na ku-organize kundi la watu waliomuibia mashairi ya nyimbo
hizo 3,000.
Habari hii ya kweli inaweza kuchukuliwa kama
sehemu ya ucheshi kwa wote waliotajwa lakini Dupree yuko serious.
没有评论:
发表评论