Tamasha kubwa la watoto ‘Extreme
Kids Festival’ litakalofanyika May 31 na June 1 katika viwanja vya Leaders
Club, Dar es Salaam na litapambwa na mwimbaji mkongwe wa kike anaependwa sana,
Lady Jay Dee.
Lady Jay Dee atajumuika na watoto
watakaohudhuria tamasha hilo, atawaongoza kuimba nyimbo mbalimbali ili
kuwahamasisha kuonesha vipaji vyao na atawapa zawadi wale watakaofanya vizuri
zaidi.
“Watoto Mambo vipi, Jay Dee
nawakaribisha watoto wote pamoja na wazazi na walezi. Mje basi katika Extreme
Kids Festival. Ni Jumamosi ya tarehe 31 May, si hapo tu na Jumapili ya
tarehe 1 June. Tunatoa nafasi kwa watoto kuzindua vipaji vyao vya kuimba na
washindi watapata zawadi.” Amesema Lady Jay Dee kwenye maelezo yake.
Katika tamasha hilo, mbali na
michezo/games mbalimbali inayopendwa zaidi na watoto pia kutakuwa na semina
fupi kwa ajili ya wazazi na walezi kwa ajili ya kuboresha malezi ya watoto.
Kutakuwa pia na bidhaa mbalimbali
huduma muhimu bora zaidi kwa ajili ya watoto na wanafamilia zitatolewa kwa siku
hizo mbili.
Waandaaji wa Extreme Kids Festival
wamesisitiza kuwa kutakuwa na usalama wa kutosha kwa ajili ya watoto na wote
watakaohudhuria na kwamba hakutakuwa na pombe .
没有评论:
发表评论