Mume wa muimbaji wa injili Flora
Mbasha, Emmanuel Mbasha ambaye pia ni muimbaji anatafutwa na jeshi la polisi
kwa tuhuma za kumbaka shemeji yake mwenye umri wa miaka 17.
Kwa mujibu wa Global Publishershers,
mwanaume huyo anasakwa na jeshi la polisi baada ya shemeji yake kuripoti katika
kituo cha polisi Jumatatu wiki hii majira ya mchana na kufungua mashitaka dhidi
ya mwanaume huyo akidai kuwa alimmbaka kwa nyakati tofauti katika siku mbili
(Ijumaa na Jumapili) ya wiki iliyopita nyumbani kwa Mbasha, Tabata-Kimanga, Dar
es Salaam.
Imeelezwa kuwa mlalamikaji
alifanyiwa kitendo hicho Jumamosi sebuleni kwa Mbasha, na Jumapili ndani ya
gari la mlalamikiwa na kwamba kutokana na maumivu makali aliyosababishiwa
aliamua kuripoti katika kituo cha polisi na kufungua kesi yenye Kumbukumbu Na.
TBT/RB/3191/2014 na ya Jalada la Uchunguzi Na. TBT/IR/1865/2014.
Taarifa hizo zimeeleza kuwa kulikuwa
na ugomvi mkubwa kati ya Flora na mumewe hali iliyomsababiha Flora kuondoka
nyumbani na kuishi hotelini na nafasi hiyo mumewe aliitumia kufanya tukio hilo.
Global Publishers imeeleza kuwa
ilizungumza na mlalamikaji kwa njia ya simu na alithibisha kufanyiwa kitendo
hicho na mume wa Flora na kueleza kuwa tayari wameshatoa taarifa polisi.
Hata hivyo, tangu kuwepo na tuhuma
hizo mwimbaji huyo wa kike hajapost chochote kwenye Facebook.
Jeshi la polisi bado halijatoa tamko
rasmi kuhusu tukio hilo.
没有评论:
发表评论