Hatimaye Jay Z, Beyonce na mdogo
wake Solange wametoa tamko rasmi kuhusu ugomvi uliotokea kwenye lift na video
yake kusambaa kwenye mitandao ikimuonesha Solange akimpiga makofi na mateke Jay
Z.
Watatu hao waliandika tamko lao na
kulituma kwa Associated Press, May 15.
Wanafamilia hao kwa pamoja wameeleza
katika tamko lao kuwa wameyamaliza matatizo yote kama wanafamilia na kwamba ni
kawaida kwa familia zote kugombana na wao ni sehemu ya familia hizo pia.
“Kutokana na press release
iliyotolewa ya video ya tukio lilitokea kwenye lift kuanzia Jumatatu, May 5,
kumekuwa na usambaaji mkubwa wa maelezo kuhusu nini kilisababisha tukio hilo.
Lakini kitu cha muhimu zaidi ni kwamba familia yetu imeshalishughulikia na
limeisha.
“Jay na Solange kila mmoja amechukua
jukumu lake kwa kile kichotokea. Wote wametambua nafasi yao waliyohusika katika
hili suala la faragha ambalo limetolewa hadharani. Wote wameombana msamaha na
tunaendelea mbele kama familia iliyoungana.” Wameandika katika tamko hilo.
Hata hivyo wamekanusha ripoti
zilizoeleza kuwa katika siku hiyo Solange na alikuwa amelewa sana na kwamba
muda wote alikuwa akionesha tabia sizizo za heshima.
“Mwisho wa siku familia zote zina
matatizo na sisi hatuko tofauti. Tunapendana na zaidi ya yote sisi ni familia.
Tumeliweka hili nyuma na tunatumaini mtu mwingine yeyote pia atafanya hivyo
pia.”
Bado tetesi za chanzo cha ugomvi wao
zinaelezwa kuwa ni kitendo cha Jay Z kuonekana anakuwa na ukaribu sana na
mwanamitindo Rachel Roy kitu ambacho hakikuwafurahisha Beyonce na Solange.
Chanzo kimeliambia New York Daily
News kuwa kitu kilichopandisha hasira za Solange zaidi ni pale Jay Z alipotaka
kwenda kwenye after party ya Rihanna bila Beyonce na ikaonekana kama ataenda na
Rachel Roy.
没有评论:
发表评论