DIAMOND PLATINUMZ ATISHA KTMA TUZO 7 ZAKE , ORODHA KAMILI YA WASHINDI IPO HAPA.
Tuzo za Muziki za Tanzania zinazodhaminiwa na
bia ya Kilimanjaro (KTMA2014), zilifanyika jana katika ukumbi wa Milimani City,
Dar es Salaam ambapo Diamond Platinumz aling’aa zaidi na kuweka historia kwa
kuondoka na tuzo saba.
Ulikuwa usiku mzuri kwa mwimbaji huyo ambaye
alishinda kila kipengele alichokuwa anashindania na hivyo kumfanya aweke
historia nzuri katika muziki wake na kudhibitisha kuwa ndiye msanii anayefanya
vizuri/anaependwa zaidi Tanzania.
Diamond alishinda tuzo ya Video bora ya mwaka
(My Number One), Muimbaji bora wa kiume-Kizazi kipya, mtumbuizaji bora wa kiume
–Kizazi kipya, Mtunzi bora wa mwaka – Kizazi Kipya, Wimbo bora wa Afro
Pop, Wimbo bora wa mwaka na Wimbo bora wa kushirikiana alioshirikishwa na
Nay wa Mitego (Muziki Gani).
Diamond alipewa kampani mara zote na mchumba
wake Wema Sepetu ambaye alikuwa kivutio kwa mashabiki wao kila alipopanda nae
jukwaani.
Kwa upande wa hip hop ambao huvuta umakini na
msisimko wa watu wengi kutokana na ushindani mkubwa, ulikuwa mzuri mwaka huu
kwa rapper wa Mwanza Fid Q ambaye kwa mara ya kwanza alishinda tuzo mbili.
Ngosha aliondoka na tuzo ya Msanii bora wa Hip Hop na mtunzi bora wa
mwaka –hip hop.
Kundi la Weusi pia lilibeba tuzo mbili ambazo
ni Kikundi cha Mwaka cha Kizazi Kipya na Wimbo bora wa mwaka (Nje ya Box-
Nikki wa Pili feat. Joh Makini &G-Nako).
Rapper Young Killer pia alifanikiwa kuibeba
tuzo kwa mara ya kwanza ambapo alishinda tuzo ya Msanii bora anayechipukia.
Kwa upande wa Bendi, mwanamuziki kutoka
Congo, Christian Bella alikuwa sura mpya katika tuzo hizo mwaka huu na
aliondoka na tuzo ya Mtunzi bora wa mwaka.
Tuzo hizo zilipambwa na burudani safi toka
kwa wasanii mbambali walioonesha uwezo wa hali ya juu ya kutumbuiza; Mwana FA,
Kundi la Weusi, Vanessa Mdee, Makomando, Madee, Ommy Dimpoz, Diamond, Meninah,
Angel, bendi za Extra Bongo na Twanga Pepeta na wengine.
Angalia orodha kamili ya washindi
KTMA2014:
Wimbo bora wa mwaka
Number One – Diamond
Mwimbaji bora wa kike – kizazi kipya
Lady Jaydee
Muimbaji Bora wa kiume – Kizazi Kipya
Diamond
Muimbaji bora wa kike taarab
Isha Ramadhan
Muimbaji Bora wa kiume – Taarab
Mzee Yusuf
Muimbaji bora wa kiume – Bendi
Jose Mara
Muimbaji Bora wa Kike – bendi
Luiza Mbutu
Msanii Bora wa Hip Hop
Fid Q
Msanii Bora Chipukizi Anayechipukia
Young Killer
Rapa Bora wa Mwaka – Bendi
Furguson
Mtumbuizaji bora wa kike muziki
Isha Ramadhani
Mtumbuizaji bora wa kiume wa muziki
Diamond
Mtunzi Bora wa Mwaka – Hip Hop
Fid Q
Video Bora ya Mwaka
Number One – Diamond
Bendi ya Mwaka
Mashujaa Band
Kikundi cha Mwaka cha Taarab
Jahazi Modern Taarab
Kikundi cha mwaka cha kizazi kipya
Weusi
Mtayarishaji bora wa nyimbo wa mwaka
– Taarab
Enrico
Mtayarishaji bora wa nyimbo wa mwaka
– Kizazi kipya
Man Walter
Mtayarishaji bora wa nyimbo wa mwaka
– Bendi
Amoroso
Mtunzi Bora wa Mwaka – Taarab
Mzee Yusuf
Mtunzi Bora wa Mwaka – Kizazi Kipya
Diamond
Mtunzi Bora wa Mwaka – Bendi
Christian Bella
Wimbo bora wa Kiswahili – Bendi
Ushamba Mzigo – Mashujaa Band
Wimbo bora wa reggae
Niwe na Wewe – Dabo
Wimbo bora wa Afrika Mashariki
Tubonge – Jose Chameleone
Wimbo bora wa Afro Pop
Number One – Diamond
Wimbo bora wa Taarab
Wasiwasi Wako – Mzee Yusuf
Wimbo bora wa Hip Hop
Nje ya Box – Nick wa Pili f/ Joh Makini
& G-Nako
Wimbo Bora wa R&B
Closer – Vanessa Mdee
Wimbo Bora wa Kushirikiana
Muziki Gani – Nay wa Mitego ft Diamond
Wimbo bora wa ragga/dancehall
Nishai – Chibwa f/ Juru
Wimbo bora wa zouk /rhumba
Yahaya – Lady Jaydee
Hall of FAME Award
Hassan Rehani Bichuka
Masoud Masoud & TBC Taifa
没有评论:
发表评论