Imeelezwa kuwa Kim Kardashian na
Kanye West wamebadili eneo watakalofungia ndoa yao kutoka Paris Ufaransa na
sasa watafunga ndoa hiyo Florence, Italia May 24.
Chanzo cha karibu na wanandoa hao
watarajiwa kimeiambia ET kuwa wawili hao wamepanga kula chakula cha usiku na
wageni huko Paris, Ufaransa kabla ya ndoa na baadae watawasafirisha wageni wote
waalikwa kwa ndege binafsi kuhudhuria sherehe ya ndoa yao huko Italia.
Jumamosi, familia ya Kardashians
ilimfanyia Kim K ‘bridal shower’ huko Baverly Hills, California.
Hivi karibuni kupitia twitter, Kim K
alikanusha habari kuwa wameshafunga ndoa ya kisheria na kwamba bado orodha ya
wageni waalikwa haijawekwa wazi na inayoonekana sio ya kweli.
Alizikana pia
picha za shela zinazooneshwa na kuaminika kuwa ni shela atayoivaa.
Kim Kardashian na Kanye West
walikuwa katika uhusiano wa mapenzi tangu mwaka 2012 na walichumbiana October
2013.
没有评论:
发表评论