50 CENT ASEMA ALBUM NZIMA YA KANYE WEST 'YEEZUS' KWAKE SIO HIP HOP NI KAMA MUZIKI WA KAWAIDA TUU.
Kiongozi wa G-Unit, 50 Cent ameweka wazi kuwa
haipendi kabisa albam ya Kanye West ‘Yeezus’ na kwamba kwake bado anasikiliza
albam ya mwaka 2004 ya rapper huyo ‘The College Dropout’.
Rapper huyo alitoa mtazamo wake kuhusu albam
hiyo wakati akifanya mahojiano na MTV News ya U.K.
“(Kanye West) ni kipaji katika utamaduni wetu
na ni moja kati ya nguvu zinazousogeza, lakini kuna vitu vingine ni vya ajabu
kwangu.” Alisema 50 Cent.
“Record hiyo ya mwisho, niwe mkweli,
siichezi/siisikilizi sasa hivi. Bado nacheza ‘Flashing Lights’, ‘Gold Digger’
na mradi nzima ya ‘The College Dropout’. Lakini baadhi ya vitu vipya ni vya
kiubunifu sana na nahisi kama anajaribu kutengeneza sound mpya.”
“It sounds scrambled... radio is going to
play dance music, EDM - you got a lot of stuff happening in music culture
that's influencing a lot of R&B music to that tempo. It doesn't feel like
Hip-Hop to me, it feels like a fusion of something else, like a weird
combination of dance music sounds and stuff.”
50 alieleza kuwa Kanye West ni msanii, na
kwamba sio lazima ukubaliane ka kila kitu anachofanya msanii na kujitolea mfano
yeye kuwa hana msanii anaempenda zaidi lakini kuna nyakati anazozipenda zaidi
kutoka kwa wasanii.
50 Cent anajiandaa kuachia albam yake mpya
‘Animal Ambition’ ambayo inatarajiwa kuingia sokoni June 3.
没有评论:
发表评论