Lady Jay Dee anatarajia kuzindua
audio na video ya wimbo wake mpya unaoitwa ‘Nasimama’, Jumamosi, April 12.
Lakini anahitaji kuwa na mashabiki ambao watapata nafasi ya upendeleo kutokana
na kufuatilia hatua zake kimuziki.
Jana, mwimbaji huyo alitoa nafasi
kwa mashabiki 15 kushinda nafasi ya kuhudhuria uzinduzi huo bila kiingilio kwa
kujibu swali lililouliza Studio ambayo amerekodi ‘Nasimama’ na tayari ilipata
majibu sahihi kutoka kwa mashabiki hao kuwa ni Sharobaro Records.
Leo, Anaconda ameongeza swali
lingine na nafasi nyingine 15 kupitia akaunti yake ya Facebook na Twitter kwa
wale watakaoweza kutaja kampuni aliyofanya nayo video.
“Hii ni kwa walioko Dar es salaam
tu, Shughuli inafanyika Nyumbani Lounge Jumamosi April 12.
SWALI: Video ya wimbo Nasimama
imetengenezwa na kampuni gani?” Inasomeka sehemu ya maelezo ya Jide.
Kama unataka kuwa sehemu ya uzinduzi
huo kupitia nafasi hii maalum, nafasi hii inaweza kuwa yako. Uzinduzi huo
utafanyika Nyumbani Lounge.
没有评论:
发表评论