2014年4月22日星期二

WASANII WA MUZIKI WA KIZAZI KIPYA AFRIKA MASHARIKI WANAMPANGO WA KUZISUSIA TUZO ZA MTVMAMA

Website ya Nairobi News imeripoti kuwa wasanii wa Afrika Mashariki wanapanga kuzisusia tuzo za MTV Africa Music Awards, MAMA.

Wasanii hao wanazishutumu tuzo hizo kwa kutozitendea haki nchini za Afrika Mashariki mwaka huu na kwa kuwapendelea wasanii wa Afrika Kusini na Nigeria zaidi. “Uganda imeumia zaidi kwasababu kutajwa kwao pekee ni kwa collabo na Amani,” msanii mkubwa wa Kenya ambaye hakutaka kutajwa jina lake aliuambia mtandao huo.

Umeandika kuwa wasanii waliotarajiwa kutajwa kwenye tuzo hizo ni AY, Ommy Dimpoz na Lady Jaydee, Tanzania, P-Unit, STL, Elani na Wyre wa Kenya na Jose Chameleone na Navio wa Uganda. Mtandao huo umeripoti kuwa wasanii wengi zaidi wanapanga kutoshiriki kwenye show za utangulizi za Road to Mamas zitakazofanyika Dar es Salaam kwa Afrika Mashariki.


没有评论:

发表评论