Bongo Flava inalipa na inazidi
kuwatoa wasanii wengi nje ya mipaka ya Tanzania ambapo tumewasikia baadhi ya
wasanii wakubwa wakipata shows nje ya nchi.
Mwimbaji wa Roho Yangu, Rich Mavoko
ana kila sababu ya kufurahia matunda yanayoendelea kuongezeka katika shina la
muziki mzuri anaoufanya ambapo hivi karibuni ataingia barani Ulaya kufanya
shows zisizopungua nane ikiwa ni kwa mara ya kwanza anafanya show nje ya bara
hili.
“Mungu akijalia naweza nikaenda
Europe na naenda kufanya shows kama nane hivi. Kwa hiyo my manager ndio alikuwa
anahangaikia hivyo vitu…vitu vyote hivyo yeye ndiye anafanya. Kwa hiyo Mungu
awabariki, nijaribu kutoka.”
Rich Mavoko ameeleza kuwa ziara hiyo
ni matunda ya wimbo wake wa Roho Yangu ambao umempa shows nyingi zaidi ndani ya
nchi na sasa ameanza kutoka nje ya nchi, na kwamba ni wimbo mkubwa ambao yeye
pia anauheshimu sana.
Hata hivyo, mwimbaji huyo amesema
bado ni mapema kutaja nchi na tarehe rasmi atakayoondoka lakini ameshacomfirm
na anasubiri kukamilisha taratibu nyingine.
“Kuna vitu naviweka sawa. Kwa hiyo
vikishakuwa sawa nitatangaza naenda wapi na wapi. Lakini vitu viko tayari
yaani.”
Rich Mavoko anakuwa msanii wa pili
kuelekea Ulaya hivi karibuni. Ben Pol yeye atafanya show Munich, Ujerumani
April 30 mwaka huu
Credt timesfm
没有评论:
发表评论