Msanii wa muziki anayefanya poa hapa
Tanzania, AT ambaye anaiwakilisha vizuri Zanzibar katika ramani ya muziki
kitaifa na kimataifa,
amesema kuwa, kuna haja ya wadau na vyombo vya habari
kuongeza nguvu zaidi katika kutoa sapoti kwa wasanii wenye vipaji kutoka huko
Zanzibar.
Kauli hii ya AT imekuja kutokana na
hali halisi juu ya uchache wa wasanii kutoka Tanzania Visiwani wanaofanya
vizuri katika Mainstream, ambapo AT amesema, mbali na uchache wao, kuna haja ya
kuwaangalia zaidi na kutoa sapoti ili kuwafikisha juu.
Ili kufikisha wasanii na muziki wa
Zanzibar juu zaidi media na raia lazima wahusike kwa asilimia kubwa zaidi.
没有评论:
发表评论