Jina la Diamond Platinumz mtoto wa
Tandale mwenye historia ya kuishi maisha ya ukata, sasa hivi ni moja kati ya
majina makubwa kimuziki barani Afrika huku akishiriki kwenye project kubwa kama
One Campaign iliyoongozwa na D’Banj huku akipewa mashavu na wasanii wakubwa wa
Afrika Magharibi.
Dully Sykes ameuambia kati ya sababu ambazo zinambeba mwimbaji huyo na kumpeleka kwenye
level ya juu ya mafanikio kuwa ni kiu kubwa aliyonayo inayomfanya afanye kazi
usiku na mchana huku akiwasumbua maproducer bila kusubiri wamuite studio.
“Wasimuone Diamond anafanya vizuri,
Diamond anafika mbali wakafikiria Diamond anafanya kazi kwa kumsubiria hadi
producer amuite studio, no sio kweli. Diamond anashinda usiku kila siku
studio.” Amesema Dully Sykes.
Dully ameeleza kuwa hata yeye pia
hukesha studio akifanya kazi na ndio sababu inayomfanya aendelee kufanya vizuri
tangu alipoanza muziki bila kupotea na kwamba wasanii wengi wasiofanya hivyo
huishia kuporomoka na kudai kuwa walioko juu wanafanya uchawi.
Mwimbaji huyo ambaye ni mmiliki wa
studio ya 4.12 ameongeza kuwa akili ya kuwekeza kwenye vitega uchumi pindi
uwapo juu ni moja kati ya sababu zinazomsaidia msanii kuendelea kuwa juu kwa
muda mrefu.
“Kama wangekuwa wajanja sasa hivi
wangekuwa na vitega uchumi…kitu kama studio ni kama jiko. Unakula kwa kutumia
studio. Hata kama mtu haji lakini unaweza kutengeneza muziki kwa kutumia akili
yako ukasema ‘leo bwana nimeamka saa kumi ya usiku nina idea yangu hebu ngoja
niingie studio nidumbukize hii sauti pengine kesho itanifaa.
Na kweli unakaa
unapata idea nzuri na unatengeneza kitu kizuri.”
credt timesfm
没有评论:
发表评论