Wiki chache zilizopita Mr & Mrs
Carter (Jay Z na Beyonce) walitangaza kuwa hawatahudhuria harusi ya “KimYe”
(Kanye West na Kim Kardashian) itayofanyika Siku ya tarehe 24 ya mwezi ujao
sababu ya kutokutaka kuonekana katika kipindi cha ‘Keeping up with the
Kardishians’ .
Habari mpya kutoka kwa Carters
Family ni kwamba amepanga kutumia zaidi ya “£100.000″ kwa kukodi Yatch
binafsi ambayo Kanye na Kim watafanyia Honey Moon yao.
Yatch hiyo itakodiwa
kutoka katika kampuni moja kubwa huko nchini Ufaransa ambako ndipo ndoa ya
wawili hao itafanyika.
Habari nyingine kutoka kwa watu wa karibu wa Jay Z
zinasema kuwa rapper huyo anampango wa kumfanyia party kubwa rafiki yake huyo
wa karibu Kanye mara tu atapotoka katika Honey Moon yake na party hiyo
itafanyika ndani ya club anayomiliki Jay Z iitwayo club 40/40 mjini
Manhattan New York.
Kanye na Jay Z wamekua marafiki kwa
mda mrefu sana na hata KIM na Beyonce inadaiwa kuwa sio marafiki sana kihivyo.
Tovuti ya Radar Online siku chache zilizopita iliripoti kuwa Kim na Beyonce
walikutana katika CLINIC moja ya watoto huko New York lakini Beyonce alionekana
kama anampotezea Kim.
没有评论:
发表评论