2014年4月16日星期三

HABIDA; MUDA MWINGI NITAKUWA AFRIKA KUSINI KIKAZI.


. Msanii Habida kutoka nchini Kenya, ameweka wazi kuwa baada ya kusaini mkataba na lebo ya muziki ya Gallo Records ya huko Afrika Kusini, ratiba ya maisha yake imebadilika sana ambapo kwa sasa muda mwingi anakuwa huko Afrika Kusini kikazi.

Habida amesema kuwa muda mwingi amekua akiutumia kutengeneza rekodi mpya ambazo zitakuwa zinatoka kwa mipangilio kuanzia hivi karibuni.

 Habida ambaye pia pembeni ya muziki anajishughulisha na masuala ya uigizaji, anatarajia kuendelea kushine kupitia vituo vikubwa vya Televisheni Afrika kupitia ushiriki wake katika project kadhaa kubwa za maigizo huko Afrika Kusini.

没有评论:

发表评论