Mwimbaji wa Nigeria Timaya ingawa
amekiri kuwa elimu ni ufungua wa maisha bora, anaamini Elimu hiyo haipo kwa
ajili yake.
Timaya ambaye hakupata elimu ya
kutosha amekuwa na ushawishi mkubwa kwa vijana nchini Nigeria kupitia kazi yake
ya muziki
“Elimu sio kwa ajili yangu ,ni
muhimu ndio lakini sio kwa ajili yangu.”
Ameuambia mtandao wa Thenet.
Ameeleza kuwa alikata tamaa na suala
la elimu baada ya kufanya vibaya katika masomo yake wakati akiwa shuleni.
Hata hivyo amewatia moyo wale wanao
endelea na masomo na wanahisi wanauwezo wa kufanya vizuri.
“sina ubongo wa kusoma shule lakini kwa wale
ambao mnao, tafadhali endeleeni ni vizuri sana.” Ameeleza
Credit:
Julian Ishungisa
没有评论:
发表评论