Flaviana Matata amekua mwakilishi mzuri wa
Tanzania kwenye nchi mbalimbali alizofanya kazi kama Ufaransa, Hispania na
Marekani ambako anaishi sasa hivi New York.
Flaviana amethibitishwa rasmi na facebook
kwamba hiyo account yenye hicho kitiki hapo juu ndio account yake pekee na
halali hivyo ule utapeli ambao ulikua unafanywa kwa kutumia account nyingine
feki za Flaviana utaishia hapa.
Flavvy anakua Mtanzania wa kwanza
ninaemfahamu kuwa verified na facebook ambapo tayari kwenye account yake ya
twitter yuko verified pia ambapo Watanzania wengine ambao wako verified twitter
ni President Jakaya, Hasheem, Ay, mawaziri January Makamba na Lazaro Nyalandu.
没有评论:
发表评论