JAGUAR AMERUDI GEREZANI KUWASHUKURU WAFUNGWA MARA BAADA YA VIDEO YAKE KUFANYA POA.
Baada ya kufanya poa kwa video ya msanii
JAGUAR ijulikanayo ka ‘Kioo’. Msanii huyo ameamua kurudi katika gereza
la Industrial Area nchini Kenya na kutoa shukrani kwa wafungwa wa gereza
hilo kwani video yote ya Kioo ilifanyika ndani ya gereza
hilo.
Katika video aliyoweka kupitia akaunti yake ya Instagram Jaguar
aliwashukuru wafungwa hao akisema “Mnakumbuka ile video tuliifanya
apa Kioo? Io ngoma imekuwa kubwa sana na ndo maana nimerudi kusema asanteni
sana.”
Jaguar alisindikizwa na Nonini na Bahati
ambaye anatamba sana kwa upande wa wasanii wanaoimba Gospel Kenya. Mwisho wa
siku Jaguar, Nonini na Bahati walidondosa show ya nguvu kwa wafungwa hao.
没有评论:
发表评论