Kundi la Wagosi wa Kaya kutoka Tanga
ambalo liliwavuta mashabiki wengi Tanzania kwa nyimbo zenye ujumbe wa maisha
halisi ya Kitanzania mwaka 2001 walipotoa album ya Ukweli Mtupu, limepanga
kurudi tena mwaka huu.
Kundi hilo linaloundwa na Mkoloni na
Dr. John, limeanzisha ukurasa mpya wa Facebook ikiwa ni sehemu ya miradi ya
ujio wao ili waweze kuwa karibu zaidi na mashabiki wa sasa ambao wengi wako
kwenye mitandao ya kijamii.
“BAADA YA KUTOREKODI KWA PAMOJA KAMA
KUNDI KWA MIAKA 8,SASA WAGOSI WA KAYA TAYARI TUMESHAREKODI NYIMBO KADHAA AMBAPO
WIKI HII TUNATARAJIA KUTAMBULISHA KAZI TULIZOFANYA UKIZINGATIA UKIMYA WA MUDA
MREFU ULIOKUWA UMETAWALA KATIKA MUZIKI WETU WA HIP HOP........stay tuned!”
Wagosi wa Kaya wameandika kwenye ukurasa wao wa Facebook uliopokelewa na
comments nyingi za mashabiki wanaotamani kusikia tena kutoka kwao.
Huenda ‘Gahawa’ likawa ni jina la
wimbo wao mpya kwa kuwa ndio jina liliwekwa mbele kwenye picha yao ya pamoja.
Post nyingine za Wagosi wa Kaya
zinaonesha kuwa audio za nyimbo zao zitaambatana na video. Endelea kufuatilia
tovuti ya Times Fm na kusikiliza 100.5 Times Fm uwe wa kwanza kufahamu hatua
wanazopiga Wagosi wa Kaya mwaka huu.
Soon tutaongea na bwana Fredrick G
Mariki ‘Mkoloni’ na John E Simba ‘Dr. John’ kuhusu ‘Gahawa’ na mengine mengi
没有评论:
发表评论