Muigizaji wa bongo movie, Wema
Sepetu alipigiwa kura nyingi zaidi na wasomaji wa gazeti la Ijumaa na hivyo
kuibuka mshindi kwenye shindano la kumtafuta msichana mwenye mvuto zaidi
(Sexiest girl) lililoendeshwa kupitia gazeti hilo.
Wema alitangazwa rasmi Jumapili
(April 20) uwanja wa Dar Live katika show iliyoandaliwa na Global Publishers.
Kwa mujibu wa kura za wasomaji wa gazeti hilo, Wema aliwafunika Jackline
Wolper, Jokate Mwegelo, Nelly Kamwelu na Elizabeth ‘Lulu’ Michael.
Tamasha hilo la kumtangaza msichana
mwenye mvuto zaidi liliambatana na show kali ya kundi la Weusi na kundi la
Mkubwa na Wanae.
没有评论:
发表评论