SABABU ZA IZZO B KUTOKENDA KUMPIGIA KAMPENI RIDHIWANI KIKWETE WAKATI NI MTU WAKE WA KARIBU, SOMA HAPA..
Jumapili iliyopita (April 6), Ridhiwani
Kikwete alitangazwa na tume ya Taifa ya Uchaguzi kuwa mshindi wa kiti cha
ubungo wa jimbo la Chalinze mkoani Pwani.
Hii ilikuwa habari njema pia kwa Izzo Bizness
ambaye aliwahi kumuimbia mbunge huyo ambaye ni mtoto wa Rais Kikwete akimtaka
aongee na ‘mshua’ kuhusu hali halisi ya mtaani.
Izzo Bizness ameuambia mtandao wa Bongo5 kuwa
tangu atoe wimbo huo amekuwa karibu na Ridhiwani kimawasiliano na hata wakati
wa kampenzi za ubunge wa jimbo la Chalinze alimuomba amsaidie lakini alishindwa
kufanya hivyo kutokana na hali ilivyokuwa kwa upande wake.
“Kuna vitu vidogo tu ambavyo tulipishana,
niliangalia pia katika upande wangu. Hakikuwa kitu cha kusaidiana kimasihala
kwa kuwa unapoamua kuingia kwenye kampeni kumsaidia mtu ujue ushaamua kutake
risk. Na hapo mimi nilikuwa naenda kukipa tafu chama cha CCM lakini mimi
natokea jimbo ambalo limeshikiliwa na CHADEMA na wananchi asilimia kubwa ni
CHADEMA”. Amesema Izzo Bizness
没有评论:
发表评论