March 20 2014 Waziri mkuu wa Australia alitangaza bungeni kwamba nchi
yake kupitia picha za satellite imeona vipande kwenye bahari ya hindi
ambavyo vinaaminika kuwa mabaki ya ndege ya Malaysia iliyopotea ikiwa na
abiria 239 March 8 2014.
Saa kadhaa baada ya hizo taarifa kutoka, ilitangazwa kwamba vikosi
vya uokoaji vimeshindwa kufika kwenye eneo hilo la tukio baharini
kutokana na hali mbaya ya hewa iliyochangiwa na mvua.
Leo
March 21 2014, taarifa kutoka vyombo vikubwa mbalimbali vya habari
duniani, imefahamika hakuna kilichoonekana eneo la tukio kwenye bahari
ya hindi ambako ‘ilisemekana’ vipande vya ndege hiyo iliyopotea
vimeonekana hivyo vikosi vya uokoaji vimeondoka eneo hilo.
没有评论:
发表评论