Maandalizi ya Harusi ya Paul Okoye
kutoka P Square pamoja na mpenzi wake Anita Isama, ambayo itafanyika
tarehe 22 mwezi huu huko Port Harcourt Nigeria, yameanza kushika kasi
ambapo mbali na mambo mengine, zoezi la kusambaza kadi kwa waalikwa
maalum wa sherehe hii, tayari limeshaanza.
Harusi hii inatarajiwa kuweka rekodi
nyingine ya aina yake, na hii ni kutokana na dalili za awali kabisa,
ikianziwa na ufahari wa kadi yenyewe ya harusi ambayo tayari
imekwishaonekana hadharani.
Paul na Anitha waliingia katika uchumba
rasmi mwezi Septemba mwaka jana, na tayari wana mtoto mmoja wa kiume
ambaye anatambulika kwa jina Andre.
没有评论:
发表评论