Bado hakuna majibu yoyote yaliyoanza kupatikana kuhusu ilipo ndege ya shirika la Malaysia aina ya Boeing 777 iliyopotea kimaajabu siku tatu zilizopita ingawa juhudu kubwa zinaonekana kuongezwa na Malaysia na nchini nyingine kubwa katika msako huo.
Lakini kinachowaumiza kichwa FBI na maafisa wa Malaysia ni watu wawili waliosafiri na ndege hiyo kwa kutumia tiketi za wizi na tayari imeonekana kuna mtu mmoja ambaye alienda kuzinunua tiketi hizo ambaye hata hivyo hajatambulika.
Tiketi hizo ziliibiwa kutoka kwa raia wa Australia na raia wa Italia. FBI inaendelea kuangalia alama za vidole za watu hao katika kumbukumbu zao, alama zilizochukuliwa katika uwanja wa ndege wa Kuala Lumpur.
Haijajulikana sababu za watu hao kupanda ndege hiyo kwa tiketi ya wizi na utambulisho wao halisi.
Afisa wa jeshi la maji la Marekani (Navy), William ameiambia CNN kuwa bado ni mapema kufahamu sababu ya ndege hiyo kupotea lakini wapelelezi wanaendelea kupima uwezekano wowote unaoweza kuchukuliwa kama sababu lakini bado hisia za ugaidi kuwa chanzo ziko mezani zinafanyiwa kazi japo maafisa wa kiintelijensia wamedai kuwa kuna uwezekano mdogo wa ugaidi.
Ndege hiyo ilikuwa inaelekea Beijing, China na ilikuwa na abiria 239 na kati ya hao raia wa China walikuwa 154.
没有评论:
发表评论