Samwel Sitta amechaguliwa kuwa mwenyekiti wa bunge maalum la katiba kwenye uchaguzi uliofanyika leo jioni mjini Dodoma
Akitangaza
matokeo hayo msimamizi wa uchaguzi huo amesema kati ya kura 563
zilizopigwa, Samwel Sitta amepata kura 487 na kumshinda Hashim Rungwe
aliyepata kura 69 huku kura saba zikiharibika.
Kesho
atachaguliwa makamo wa mwenyekiti wa bunge hilo ambaye anatakiwa kutoka
Zanzibar na anapaswa kuwa mwanamke kwa mujibu wa makubaliano ya wajumbe
wa bunge hilo.
没有评论:
发表评论