Pichani: Paul Walker akiwa na miwani masaa mawili kabla ya ajali
Sitaki kuuamini sana huu msemo ‘kufa kufaana’, lakini naona kama hiki ndicho kilichotokea kwa jamaa anaedai kuwa aliokota miwani ya marehemu Paul Walker aliyoonekana ameivaa saa chache kabla ya kupata ajali.
Kwa mujibu wa TMZ, muuzaji huyo anadai aliipata miwani hiyo ya jua pamoja na ‘fire extinguisher’ ambayo inasekana ilitumika katika kujaribu kuokoa maisha ya Walker na rafiki yake.
Miwani hiyo imeanza kupigwa mnada jana (March 13) kwa bei ya kuanzia $605, na mnada unafanyika kwa njia ya mtandao kupitia BidAmi.com
没有评论:
发表评论