Mamlaka ya Mawasiliano nchini -TCRA- imekipa onyo kituo cha
utangazaji cha Radio Free Afrika kutokana na kupiga muziki wa rapper
wa Tamaduni music, Nash Mc kwa madai kuwa wimbo huo ni mahudhui ya
uchochezi.
Mwenyekiti wa Kamati ya Maudhui wa mamlaka hiyo Magreth Mnyagi amesema hayo leo jijini Dar es salaam wakati akitoa hukumu juu ya kosa hilo.
Amesema kosa hilo ni la ukiukwaji wa kanuni za utangazaji za mwaka 2005 hivyo kamati imefikia maamuzi hayo baada ya kushauriana na kamati ya maudhui ya vipindi vya radio kutoka TCRA.
Bi Magreth amesema wimbo huo ulichezwa June mwaka jana. Kwa kuzingatia kauli hiyo inawezekana wimbo ni ‘Kaka Suma’, wimbo uliokuwa unazungumzia kupanda kwa nauli za daladala

没有评论:
发表评论