2014年3月27日星期四

DIAMOND PLATINUMZ ATAJWA KUWANIA TUZO ZA KORA, MPIGIE KURA KWA....

988325_625424204147144_1190455814_n
Mwaka huu unaweza kua mzuri sana kwa Diamond Platnumz kwani tumeshuhudia akifanya mambo mengi makubwa, kama kupata kolabo na wasanii wakubwa na kupata kushirikishwa katika nyimbo iliyowakutanisha mastar wakubwa kutoka Afrika. Leo asubuhi kupitia website yake Diamond alitangaza kua amechaguliwa kushiriki katika Tuzo za KORA.
Tuzo hizo zilianzishwa miaka 20 iliyopita na kwa mwaka huu Diamond ndio ataipeperusha Bendera ya Tanzania. Moja ya kitu alichokisema kupitia website yake ni jinsi utavyoweza kumsadia kushinda tuzo hizo. Diamond alisema “Tuzo kubwa za Afrika,KORA zimewadia..na mimi nahusika…hivyo basi kama mpenzi na shabiki wa Music wangu Niwezeshe kushinda kwa kunipigiakura kura . ingia katika Facebook page yao ambayo ni Kora Awards kisha Katika kila post niliyoshiriki Comment kwa kuandika jina Diamond Platnumz”
10012600_361394690666355_1624596457_n

没有评论:

发表评论