Rapper Kanye West ameamriwa na mahakama ya Los Angeles kufanya kazi za jamii kwa kipindi cha masaa 240 na kuwa chini ya kipindi cha matazamio ‘probation’ kwa miaka miwili kutokana na tukio la kumshambulia mpiga picha.
Kesi hiyo ilifunguliwa kutokana na tukio alilofanya mwezi July mwaka jana ambapo alimshambulia mpiga picha aliyejaribu kumpiga picha katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Los Angeles.
Kabla ya kutoa hukumu hiyo, ilielezwa kuwa kutokana na uchunguzi imeonekana kuwa July 19, 2013 mpiga picha anaejulikana kama Daniel alikuwa amesimama katika uwanja huo wa ndege akimsubiri Kanye West, na alipomkaribia alimuuliza kama anaweza kuongea nae.
Daniel alipoona Kanye yuko kimya akauliza swali lingine, ‘Kwa nini hatuwezi kuongea na wewe?’ Swali ambalo lilitokana na kauli ya Kanye West wiki kadhaa zilizopita kuwa hataki paparazzi amuengeleshe wala mtu yeyote.
Imeelezwa kuwa Kanye West aliweka begi chini akamfuata Daniel kama anataka kuongea nae vizuri na kisha bila kughafirishwa na neno lolote toka kwa Daniel alimvamia na kumshambulia huku akijaribu kumnyang’anya kamera yake.
Kutokana na purukushani hizo Daniel alianguka chini huku akiwa ameishikilia kamera yake na kuumia magoti na ‘hip’ na kupata maumivu makali. Alipelekwa hospitalini na Ambulance ambako aliwekwa katika chumba cha dharura.
Mahakama pia imemhukumu Kanye West kuhudhuria vipindi 24 vya daraja la pili la program ya kudhibiti hasira.
Hata hivyo Kanye West hakuwa mahakamani hapo na hivyo anatakiwa kuripoti polisi jijini Los Angeles. Kesi hiyo imepangwa kusikilizwa tena July 17 mwaka huu.
没有评论:
发表评论