‘Chuna buzi cafe’ ni moja kati ya jina la mgahawa wa msanii
kutoka hapa bongo, wa kuitwa Shilole Mohamed a.k.a Shishi baby ambaye
anakomaa na jiji ambapo anatarajia kufungua mgahawa wake wa chakula
maeneo ya nyumbani kwao Mwananyamala jijini Dar es Salaam.
Shilole akizungumza na Clouds fm leo ameelezea kwa kuwa ana taaluma
ya Hotel Management na pia mama yake alishawahi kuwa ‘mama ntilie’
kipindi cha nyuma na pia Shilole ameshawahi kufanya kazi Peacock Hotel,
Florida, na kwa sasa kila kitu kinaenda sawa ni yeye tu mwenyewe wakati
wowote anaweza akafungua.
没有评论:
发表评论