Swali ambalo wengi wamekuwa wakijiuliza hasa wadau wa muziki kuhusu kutofanya vizuri ama kubuma kwa wasanii wengi wanaojiondoa/wanaoondolewa katika kundi la Tip Top Connection limepata majibu kutoka kwa Menaja wa kundi hilo, Babu Tale.
Babu Tale alilijibu swali hilo wakati anazungumzia uamuzi wa Dogo Janja kuuomba msamaha uongozi wa Tip Top hapo jana kupitia vyombo vya habari.
“Uongo, mwenyezi Mungu hapendi uongo katika jamii, tunafanya kazi lakini mtu anapoondoka kwenye kundi akawa muongo mwenyezi Mungu anamhukumu wala sio mimi.” Babu Tale ameiambia Tovuti ya Times Fm.
“Uongo ni kitu kibaya sana.” Amesisitiza Babu Tale. “Hamna msani aliyekuja Tip Top na milioni moja yake anaanza muziki. Kila mtu kaja Tip Top hana kitu, akiondoka tu anaanza ‘Babu Tale mwizi, Babu Tale Kanidhulumu, Babu Tale tapeli.” Ameeleza.
Babu Tale ameoneshwa kushangazwa na kusikitishwa sana na kauli za wasanii hao wanaoondoka Tip Top Connection na kuwataka kuwa wakweli wanapotoka kwenye kundi hilo.
“Huyu Tapeli asiyefungwa na dhuluma, dhuluma gani hii…mimi nasimama kwenye haki ndio maana wao wanayumba mimi niko pale pale, ukisimama kwenye haki utaonekana na haki yako itaonekana.
Lakini ukisimama kwenye uongo siku zote kwenye ukweli uongo hujitenga.” Tunamkariri Babu Tale.
Wasanii ambao walitoka Tip Top na mambo yao hayakwenda sawa ni pamoja na Z-Anto, MB Dogg na Dogo.
Credit: Moko Biashara (Times Fm)
没有评论:
发表评论