Wakati jitihada za kumtibu Chris Brown ili aweze kudhibiti hasira zake zikiendelea, imeripotiwa kuwa mwimbaji huyo amefukuzwa Rehab na kuishia kwenye mikono ya polisi waliompeleka moja kwa moja polisi na kumtupa lupango.
Kwa mujibu wa ripoti za kitengo cha polisi cha Los Angeles, Chris Brown alikamatwa Ijumaa (March 14) baada ya kufukuzwa Rehab japo sababu za kufukuzwa Rehab hazikuwekwa wazi.
Kitengo hicho cha polisi kimeeleza kuwa Chris alikamatwa majira ya saa nane mchana na kwamba alitoa ushirikiano kwa polisi hao hadi alipofikishwa katika kituo cha polisi ambako aliwekwa mahabusu.
Kitengo hicho kimeeleza kuwa amekamatwa kwa warrant iliyotolewa kutokana na makosa ya kutumia silaha na kutishia katika tukio lililotokea February 7, 2009. Na pia kwenda kinyume na masharti ya probation iliyohusu kesi hiyo.
Huenda tarehe iliyotajwa na polisi imechanganywa kwa kuwa Chris alimpiga Rihanna February 8, 2009.
Hii sio mara ya kwanza kwa Chris kufukuzwa Rehab kwa kuwa aliwahi kufukuzwa baada ya kurusha jiwe lilipasua kioo cha dirisha la gari la mama yake.
Inasemekana kuwa wakati akiwa Rehab alianzisha uhusiano na mfanyakazi wa Rehab na huenda ndio chanzo cha kumuacha Karrueche Tran, japo hiyo sio sababu iliyompelekea kufukuzwa
没有评论:
发表评论