Taarifa
zilizotufikia hivi punde katika chumba chetu cha habari inaelezwa kuwa
Mkuu wa Mkoa wa Mara John Gabriel Tupa, amefariki dunia mda huu katika
hospitali ya Tarime.
Habari
zinasema kuwa umauti huo umemfika baada ya Presha kupanda ghafla
akitoka Musoma kuelekea Tarime kufunga Mafunzo ya Mgambo, ambapo
alipelekwa haraka katika hospital ya Tarime.
Katibu
wa Mkoa Bw. Benedictor, amesema kuwa wakati alipokuwa akiwasiliana na
Dokta wa hospital hiyo kila muda, aliambiwa hali ya mgonjwa inaendelea
kuimarika na baada ya muda taarifa zilizokuja zilikuwa za kifo.
Mpaka sasa mwili wa marehemu unachukuliwa kurudihwa Mkoa wa Mara ambapo alipokuwa anaishi.
Mungu ailaze roho ya marehemu mahala pema peponi Amen
CREDT DJ SEK
没有评论:
发表评论