Billboard wamemtaja Taylor Swift kuwa mwanamuziki aliyeingiza kiasi kikubwa zaidi cha pesa kupitia kazi zake za muziki mwaka 2014 ambapo anatajwa ingiza karibu dola Milioni 40 ( $39,699,575.60) katika kipindi cha miezi 12 iliyopita.
Mwimbaji huyo ameingiza kiasi hicho kutokana na mauzo ya albam yake ya mwaka 2012 ‘Red’, na mauzo ya nyimbo zake kwenye mitandao kwa kudownload. Lakini amepata kiasi kikubwa zaidi cha pesa kupitia ziara ya albam yake ‘Red’ ambayo imemuingizia kiasi kinachokadiriwa kufikia dola milioni 30.
Katika orodha hiyo iliyotolewa jana (March 10) na Billboard, Taylor Swift anafuatiwa na mkali wa Country, Kenny Chesney alyeingiza dola 32,956,240.70 alizozipata kupitia albam yake ya ‘Life on a Rock’ na ziara yake aliyoipa jina la ‘No Shoes Nation’.
Justin Timberlake ametajwa katika nafasi ya tatu akiwa ameingiza dola 31,463,297.03 alizoingiza baada ya kuachia albam mbili za ‘The 20/20 Experience’ na ‘The 20/20 Experience -2 of 2’, na ziara za albam zote mboli.
Hii ndio orodha nzima ya waimbaji 10 waliongiza kiasi kikubwa zaidi cha pesa kupitia kazi zao mwaka 2014 (katika kipindi cha miezi 12 iliyopita).
Hii ni orodha kamili ya waimbaji 10 walioingiza pesa nyingi zaidi katika kipindi cha miezi 12 hadi jana.
1. Taylor Swift - $39,699,575.60
2. Kenny Chesney - $32,956,240.70
3. Justin Timberlake - $31,463,297.03
4. Bon Jovi - $29,436,801.04
5. The Rolling Stones - $26,225,121.71
6. Beyonce Knowles - $24,429,176.86
7. Maroon 5 - $22,284,754.07
8. Luke Bryan - $22,142,235.98
9. Pink - $20,072,072.32
10. Fleetwood Mac - $19,123,101.98
没有评论:
发表评论