Msanii H baba amevunjiwa kioo kidogo cha gari lake na kuibiwa
vitu vilivyokuwa ndani leo kariakoo katika mtaa wa Lumumba, vitu
alivyoibiwa ni ikiwemo flash ambayo ina nyimbo zake, huku wezi hao baada
ya kukomba kila kitu wamenza kuvujisha ngoma zake na moja kati ya ngoma
iliyovuja ni Tubebane.
Aliandika Hivi Instagram “Wezi wamevunja Kioo
kidogo wamenikombea kila kitu mpaka nyimbo zangu . #wameanza kuvujisha
ngoma zangu nimeskia Wimbo Wangu wa #Tubebane umeenea kila Kona naombeni
mliochukua vitu vyangu naombeni nirudishieni #flash yangu au msivujishe
ngoma zangu hii nimeiskia ya #Tubebane please please msifanye hivyo
vitu bebeni haina neno ila flash yangu tuu. Ilikuwa maeneo ya kariakoo
mtaa wa rhumumba.
”
没有评论:
发表评论