Kuna mtu mmoja muhimu kwenye muziki aliwahi kunipigia simu na kuniuliza
swali hili.. Hivi kama Diamond Platnumz bahati mbaya Mungu akimchukua,
ni msanii gani mwingine wa Tanzania anayeweza kufanya anachokifanya yeye
kwa sasa na jinsi anavyoitangaza Tanzania?’ Sikumbuki nilimpa jibu
gani.. lakini Diamond Platnumz anaweza kuwa na jibu zuri kwa mtu huyu.
“Moja ya watu ambao naamini hata NIKIFA kesho, Roho yangu itakuwa na
amani ya kuamini kwamba kuna mtu ambae anaipeperusha vyema bendera ya
Nchi yangu kupitia muziki… you jus call him @ommydimpoz ila wacha mi
nimuite Kibonde,” Diamond ameandika kwenye Instagram kwenye picha ya
Ommy akiwa amesimama pembeni ya gari la kifahari aina ya Lamborghini
wakati akishoot video ya wimbo wake mpya na muongozaji maarufu wa video
Afrika, Moe Musa.
没有评论:
发表评论