2014年3月13日星期四

PICHA HIZI ZINARUDISHA TETESI ZA KURUDIANA KWA RIHANNA NA DRAKE.

article-0-12804583000005DC-500_634x416Kwa muda mrefu sasa kumekuwepo na tetesi za wanamuziki Drake na Rihanna kwamba wamerudisha mahusiano yao ya kimapenzi.

Ingawa wawili hao waliopachikwa jina la ‘AubRih’ (Kwa maana ya Aubrey na Rihanna) mpaka sasa wamekuwa wakisisitiza na marafiki lakini vitendo vya hivi karibuni vinaonyesha kuna kitu zaidi ya urafiki kati yao. Rihanna na amekuwa akionekana na Drake wakiongozana kwenye ziara ya kimuziki ya Drake barani ulaya.

Mara ya kwanza walionekana pamoja nchini Ufaransa, kisha Ujerumani na jana usiku walionekana pamoja jijini Manchester – England.

Na hizi ni picha za ushahidi wa wawili hao walivyokuwa wakijiachia kwenye mitaa ya jiji la Manchester usiku jana.

article-2579060-1C3C049300000578-520_634x434
Drake na Rihanna kwenye mitaa ya Manchester jana usiku


article-2579493-1C3BAD6900000578-472_634x389

没有评论:

发表评论