BAADA ya Baraza la Sanaa Taifa (BASATA),
kuondoa nyimbo ya msanii wa muziki wa kizazi kipya Madee, nyimbo inayojulikana
kwa jina la Tema mate Tuwachape, mapya yaibuka ambapo msanii huyo adai kuwa
Baraza hilo limechelewa kufanya maamuzi.
Msanii huyo amedai kuwa baraza hilo
limechelewa kufanya maamuzi hayo ya kuuondoa wimbo huo katika kinyg’aganyiro
hicho ikiwa nyimbo hiyo imeshapigwa kwa muda wa mwka mzima sasa.
Madee ametoa ushauri kwa baraza hilo
kuwa ni vyema wakaweka chombo maalumu cha kuhakiki nyimbo zao kabla
hazijapelekwa kwa mashabiki hali hiyo itasaidia kurekebisha makosa.
Aliongezea kuwa kuondoa wimbo huo
katika kinyanga’nyiro hicho hawajatenda haki kwani nyimbo yake imeshikiria
chati kwa muda mrefu kwenye redio mbalimbali, hivyo ni sawa na kuwadhurumu
mashabiki wake.
Alienda mbali zaidi ambapo anadai
kuwa kauli hiyo ya kuondolewa haijamshtua sana kwani hajawahi kupokea tuzo
yoyote tangu ameanza kazi ya muzi.
Nyimbo ya Madee, ni miongoni mwa
nyimbo zilizoenguliwa katika mchakato wa kinya’nganyiro cha tuzo hizo.
没有评论:
发表评论