2014年3月10日星期一

SHAKIRA; BOYFRIEND WANGU HATAKI NISHIKWE NA MWANAUME KWENYE VIDEO.


Mwanamuziki wa kike ambaye ‘hips’ zake hazidanganyi anapocheza, Shakira ameeleza kuwa chanzo cha kufanya video na Rihanna aliyemshika kama mwanaume ‘Can’t Remember to Forget You’, ni wivu alionao boyfriend wake Gerard Pique.

Katika mahojiano aliyofanya na jarida la Billboard, Shakira ameeleza kuwa mchezaji huyo wa Barcelona hataki kabisa ashikwe na mwanaume kwenye video na kwamba ni bora ashikwe na mwanamke mwenzake. Amesema kutokana na kukataliwa na Gerard, hawezi kufanya video kama alivyozoea kufanya awali na kwamba sasa inambidi afanye na wanawake.

“He’s very territorial, and since he no longer lets me do videos with men, well, I have to do them with women. It’s more than implied in our relationship that I can’t do videos like I used to.

Video ya wimbo wa Shakira aliomshirikisha Rihanna ‘Can’t Remember to Forget You’ ilikosolewa vikali katika nchi mbalimbali kwa madai kuwa inahamasisha mapenzi ya jinsi moja.

Shakira na mcheza mpira huyo wamekuwa katika uhusiano tangu mwaka 2011, mwaka jana walijaliwa kupata mtoto wa kiume na wakampa jina la Milan Pique Mebarak.

没有评论:

发表评论