Ripoti za polisi wa kimataifa ‘Interpol’ zimeeleza kuwa hakuna dalili zozote hivi sasa zinazoonesha ugaidi kuwa chanzo cha kupotea ndege ya shirika la Malaysia.
“Kadiri tunavyozidi kupata taarifa, ndivyo tunavyozidi kuhitimisha kuwa halikuwa tukio la kigaidi.” Mkuu wa kitengo cha polisi wa kimataifa Ronaldo Noble amesema katika mkutano na waandishi wa habari huko Ufaransa.
Ameeleza kuwa kwa mujibu wa wapelelezi wa Malaysia, hakuna uthibitisho wowote unaoonesha kuwa kuna connection kati ya shirika lolote la kigaidi.
Akieleza kuhusu abiria wawili waliotumia tiketi za wizi, alidai waliingia kutoka Iran na walitumia tiketi halali. Lakini pia hawakuwa na sababu za kigaidi kutumia tiketi za wizi kutoka Australia na Italia kupanda ndege hiyo iliyopotea kimaajabu.
Noble amesema tayari majina ya watu hao yameshatambulika kuwa ni Pouri Nourmohammadi (18) na Delavar Syed Mohammad Reza (29).
Polisi wa Malaysia wameeleza kuwa Noumohammadi alikuwa anaenda Ujerumani kumsalimia mama yake na kwamba hakuna dalili yoyote kuwa wasafiri hao wawili wangeweza kuwa hatari katika ndege hiyo.
Bado ndege hiyo iliyokuwa na watu 239 ikisafiri kutoka Malaysia kwenda Beijing, China haijapatikana.
没有评论:
发表评论