2014年3月13日星期四

VANESSA MDEE; RATIBA ZANGU NDIZO ZILIZOFANYA NIKATAE DEAL YA TV1

Kuna taarifa zilianza kupatikana kupitia vyanzo mbalimbali vya habari kwamba msanii ambae pia ni mtangazaji wa 102.5 Choice FM Dar es salaam Vanessa Mdee ataonekana kwenye show mpya katika kituo cha Television cha TV1.

V money anapenda kukufahamisha kwamba hatoonekana kwenye show hiyo, yani hajaichukua hiyo kazi kutokana na ratiba yake (V) kumbana kutokana na mipango yake ya sasa pia ya kusafiri kuendeleza muziki wake.

Imekua ngumu kwa sasa sababu ameamua kufocus zaidi kwenye muziki hivyo atashindwa pia kuhimili kuifanya hiyo kazi ambayo pia inaratiba kubwa ya shooting.

没有评论:

发表评论