Member wa Necessary Noise, Nazizi amekanusha taarifa zilizotolewa na mtayarishaji wa muziki wa Homeboys raia wa Tanzania Kheri Sappy kuwa ana uhusiano wa kimapenzi na mwimbaji/rapper huyo.
Sappy alitoa taarifa hizo kupitia mtandao wa Bongo5 na kuambatanisha na picha kadhaa zinazoonesha yeye na Nazizi wakiwa sehemu mbalimbali ikiwa ni pamoja na kitandani.
“Nina marafiki wengi wa kiume, tunapiga picha sehemu zote, hiyo inaonesha ninavyohusiana na rafiki zangu.” Nazizi aliiambia Nairobi News
“Kiukweli, sitashangaa nitakapoona picha nyingine zikitolewa. Kama nilivyosema, nina marafiki wengi wa kiume ambao nina ukaribu nao sana.” Nazizi alisisitiza.
Taarifa za kuwa na uhusiano wa mapenzi na Kheri Sappy zilikuja siku chache baada ya rapper huyo kuachana rasmi na mume wake.
没有评论:
发表评论